JINSI YA KUPIKA Potato wedges(Viazi vya pembe Tatu)

Kwa wale ambao wanaandaa vyakula vya sherehe mbalimbali, potato wedges zinaweza kuwa kama dish mojawapo,

Pia Unaweza kufanya kama mbadala wa chips Ili kupunguza gharama Kwa maana kwa pishi hili mtu atatumia Viazi vichache ukilinganisha na chips.

Mahitaji:

1.Viazi mbatata(Viazi vya chips)
2.Coriander(giligilani/Cotmil)
3.Kitunguu,Hoho,Caroti,Mafuta na chunvi
4.Vinegar, Soy sauce 

Jinsi ya kuandaa

1.Chukua Viazi vikubwa vimenye kisha vikate mara nne kama inavyoonekana kwenye picha, Yaani kiazi kimoja kitoke vipande vinne.

2.Kaanga Viazi kwakutumia  Mafuta mengi(Yaani Deep fry) geuza kwa kutumia mwiko na sio kijiko Ili visivunjike.

✓Hakikisha vinakauka vizuri.

Kisha chukua hoho nusu Caroti nusu na kitunguu nusu(Inategemea unaandaa kwa wingi kiasi gani).

Picha:

3.Mimi nimekuandikia kwa makadirio tu).Kisha saga kwenye blendar kwa kuweka Mafuta kiasi soy sauce kiasi na vinegar,na chunvi kiasi. 

4.Kisha huo mchanganyiko uliousaga,Weka jikoni kwenye chombo Kisha pika hadi ikauke uwe nzito kiasi(Huo mchanganyiko ukishapikwa unaitwa Sauce).

5.Chukua Coriander zikatekate vipande vigogo(Chop) alafu fuata hatua hizi hapa chini.

6.Utachukua Viazi ulivyokaanga,Utaweka kwenye chomba safi kisha utakuchua kijiko utachota Sauce utamimina juu ya Viazi

7. Kisha utaanza kuchanganya kwa kurusha rusha(mfano kama unavyopepeta Michele).

8.Utaona Viazi vimebadilika rangi Kisha utachanganya kwa kuongeza coriander.

Baada ya kufuata hatua hizo utakuwa umemaliza kuandaa POTATO WEDGES 🥔



Maoni