JINSI YA KUANDAA ROST KWAAJILI YA KUPIKA MBOGA AINA YOYOTE
- JINSI YA KUCHANGANYA VIUNGO KWAAJILI YA KUPIKA ROST
Rost la aina hii unaweza kulitumia kwaajili ya kuku,samaki,nyama nk lakini jambo moja na muhimu la kuzingatia ni kuhakikisha kwamba utaongeza kiungo mojawapo mf, Kama unapika samaki utaongeza fish masala,au Chicken masala kama unapika kuku,vilenile kama unapika Nyama basi utaongeza Beef masala
Mahitaji
Curry Powder kijiko cha chai
Chilly powder kijiko cha chai
Kitunguu swaum kijiko komoja cha chakula
Tangawizi kijiko kimoja cha chakula
Binzari manjano kijiko kimoja cha chai
Tomato paste vijiko 3 vya chakula
Galam masala kijiko kimoja cha chakula
NB,Unaweza kuongeza zaidi kipimo kutokana na wingi wa mboga unayopika
Weka viungo vyote kwenye bakuri kama vilivyoorodheshwa kisha changanya vizuri
JINSI YA KUTUMIA
Iwapo utakuwa umeshaandaa masala yako kama nilivyoelekeza hapo juu,Hatua itakayofuata ni kupika.
1.Chukua chombo safi weka mafuta
2.Mafuta yakipata moto weka kitunguu maji
3.weka kitunguu swaum na Tanzawizi
Pika kwa sekunde chache kisha weka Masala uliyoiandaa
Baada ya kuweka madsala unapika masala yako kwa dk 3 kisha uanaweka mboga yako kama ni kuku au samak,Nyama nk kisha utaogeza maji kiasi na chunvi kisha utaondoa rost lako litakuwa tayari
Imeandaliwa na Chef Shedrack
Mawasiliano 0765848756
Instagram Mpishi_Mzoefu
Maoni