JINSI YA KUPIKA CHAPATI LAINI
Mahitaji.
.Unga wa Ngano 1Kg
.Sukari 1 Kijiko cha chakula
.Chunvi 1 Kijiko cha Chakula
.Maji ya uvuguvugu
.Mafuta ya kula
NJIA.
SIRI. Hii hapa siri ya kupika chapati laini,Nikwamba Weka mafuta mwishoni kabisa yaani usiweke mafuta kwenye unga kabla ya kuweka maji.
Chukua chombo safi,Weka unga wa ngano,Kisha weka chunvi na sukari Changanya alafu weka maji ya Uvuguvugu.Endelea kuongeza maji kidogo kidogo ili maji yasizidi.
Kanda kwa muda kisha weka Mafuta.Kanda kama dk 10,Kisha funika kwa muda wa dk 20
Baada ya hapo kata Saizi ya chapati unazohitaji Alafu sukuma na kuchoma.
Wakati wa kuchomachapati,Kwenye kikaango(Frying pan) Usiweke mafuta kwanza,Ila anza kuweka chapati,
Alafu ikianza kubabuka geuza na weka mafuta upande ule uliobabuka,Kisha fanya hivyo pia kwa upande wa Pili.Usiweka mafuta kabla chapati haijababuka itatoka vibaya.
Imeandaliwa na:Mpishi Mzoefu
Ukiona posti hii,Ona Kama umekutana na Mimi Nipigie uliza Umekwama wapi? 0765848756
Maoni