Pilau rahisi halina mambo mengi fuatana nami uweze kupika mwenyewe nyumbani kwako,
Mahitaji
1.Mchele Kg 3
2.Mafuta ½Ltr
3.Vitunguu maji ½ kg
4.Kitunguu swaum ¼kikombe
5.Pilau masala 3
6.Nyama 1kg
7.Viazi ½
8.Binzari nyembamba 5
9.Ajinamoto
10.Chunvi
Mahitaji, ndo hayo kama nilivyokutangulia kusema,halina mambo mengi ila mitamu balaa,
Jinsi ya kuandaa
1.Chukua sufuria weka jikoni,Kisha weka Mafuta,Yakipata moto weka vitunguu
Kisha pika kwa kukoroga hadi viwe brown(Visiungue pilau litakuwa chungu)
2.Weka maji kikombe kimoja Ili vitunguu vibaki na rangi ya brown,visiendelee kukaangika vikaungua,Kisha weka kitunguu swaumu endelea kukoroga Kisha weka pilau Masala
3.Weka nyama,viazi koroga kisha ongeza chunvi na ajinamoto,kisha osha mchele na kuuweka endelea kukoroga
NB:Zingatia usioshe mchele au kuuloweka mapema,Mchele uoshe unapokuwa umeshafikia hatua ya kuuweka kwenye viungo Ili usinywe maji mengi Unaweza kukusumbua kwenye kupika ukatoa bokoboko.
4.Baada ya kuweka mchele weka mchuzi uliochemshia nyama uwe wa moto,Kisha koroga hadi uone pilau limekuwa zito mfano wa tope,Alafu ondoa jikoni weka pembeni
5.Ondoa mkaa jikoni,bakisha kidogo sana alafu funika pilau vizuri na foili na mfuniko kwa juu Kisha weka mkaa juu subiri
Baada ya dk30 funua alafu weka Binzari nyembamba Kisha geuza pilau,Lifunike tena kwa dakika 10.Baada ya hizo dakika pilau litakuwa tayari.
Maoni