Kuku
Hoho
Caroti
Kitunguu maji
Kitunguu swaumu
Tangawizi
Chunvi
Viazi
Jinsi ya kuandaa
Chukua kuku muoshe vizuri,weka kwenye chombo safi kisha Chukua kitunguu swaumu na tangaziwizi kiasi saga,
Chukua mchanganyiko uliousaga wa kitunguu swaum na tangaziwizi kisha changanya na kuku pamoja na chunvi kiasi na Mafuta kidogo(Marination) Acha Dk 15,
Baada ya dakika 15 mkaange kuku,Akakaule kiasi,Kisha chukua zile hoho,caroti na kitunguu vikate kwa urefu
Weka sufuria jikoni kisha weka Mafuta kiasi,weka kitunguu swaum kiasi,baaada ya hapo weka mbogamboga ulizoandaa Yaani,Hoho caroti na kitunguu
Pika hadi mboga zilainike kiasi alafu weka kuku,ongeza nyanya kidogo ya kusaga, kama huna unaweza kutumia tomato sauce,weka ndimu kiasi na soy sauce(kama unayo sio lazima)
Baada ya hatua hizo menya viazi Kisha vioshe vizuri,vikate na uvikaange hadi vikauke,
Changanya viazi pamoja na yule kuku uliye mpika,Kisha pakua,Tayari kwa kula
Maoni